KUHAMA KWA OFISI ZA NACTVET MAKAO MAKUU
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ( NACTVET) linapenda kuwataarifu wadau na wananchi kwa ujumla kuwa , Ofisi za NACTVET Makao Makuu zilizokuwa Jengo la NSSF, Ghorofa ya 3, Kilimani Dodoma, sasa zimehamia Mji wa Serikali Mtumba, Jengo la Jiji la Dodoma, Ghorofa ya 1.
Huduma zote za NACTVET Makao Makuu zitaendelea kutolewa katika Ofisi hii mpya.
Ofisi za NACTVET Kanda ya Kati Dodoma, zitaendelea na huduma zake kama kawaida katika Jengo la NSSF, Ghorofa ya 2, Kilimani.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakasababishwa na mabadiliko haya.
Kwa maelezo zaidi:
Simu bure: 0800110388de
Barua Pepe: info@nactvet.go.tz
KARIBU TUKUHUDUMIE